Taasisi ya Thrive
Kwa viongozi wanaotaka kuwa wakufunzi wa bustani hai kwenye jamii au taasisi zao. Ikihusisha nyenzo zote muhimu kwaajili ya kufanya na kufanikiwa ni pamoja na kozi 40, vyeti, mfuko kwaajili ya ukuaji na zaidi!
Hapa kuna kozi zote ambazo zimejumuishwa kwenye kifungu chako.
Kozi Zote
Mbinu za asili na endelevu (hakuna kemikali wala mbolea za viwandani) hutumika kustawisha chakula kwa kipindi cha mwaka mzima, huku ukihitaji maji kidogo. Kila bustani iliyofuata vipimo vilivyowekwa huweza kutosheleza mahitaji ya lishe kwa watu 40
Kozi Zote
Afya ni mkusanyiko wa vyakula mbalimbali. Mazao ya asili ambayo yalipandwa zamani kabla mfumo wa kupanda zao moja haujagundulika, aina mbalimbali huoteshwa kwa ujumla kama mbinu ya kuimarisha moyo,viungio na mfumo wa kinga kwa wakati mmoja.
Kozi Zote
Kila bustani hai huusisha sehemu ya mimea dawa. Hutumika kuzuia na kutibu magonjwa. Mimea hii ya asili huweza kutibu kuungua,kuhara,kudhibiti bakteria, kuzuia malaria na kutibu virusi vya UKIMWI.
Kozi Zote
Watengenezaji wa bustani hai wanapokuwa wamezalisha chakula chenye afya cha kutosha kwaajili ya familia zao, wanaweza kupeleka ziada sokoni.